DUA ZA USHINDI
-
Writen byTIMOTHY OMUSIKOYO SUMBA
- Year2023
Siku za mwambo. Msimu huo wa ukosefu wa pesa na vyakula watu waliitabika sana. Waanga wa njaa ama walilalia mate au chakula cha mshindio. Huo ndio wakati ulanguzi wa kibinadamu ulizuka. Wasiwasi ukazuka kwa watu kuhofia usalama wao. Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi ya Wahaka biashara nyeusi ya kuwanunua na kuwauza wanadamu iliingia masikioni mwa wengi. Masikio hayakuamini madai hayo kabla ya kuthibitishwa. Hata hivyo lisemwalo lipo na ikiwa halipo basi laja. Kwa hakika biashara ya walanguzi kulangua wanadamu ilivuma. Aghalabu, wakwasi au matajiri ndio walioendesha biashara hiyo. Pesa za mabwenyenye hao zilinunua watu. Mihela yao ilinunua haki za kibinadamu. Jamii isiyo na mbele wala nyuma ilitamani kuuza hata oksijeni ingawa ikawa muhali.
Awali Mwenge aliwahi kusikia tu kuhusu ulanguzi wa dawa za kulevya na zana hatari. Hilo la wanadamu kuuza wanadamu wenzao lilikuwa geni na jipya kwake. Habari zilizogonga vichwa vya habari ni kuhusu walanguzi na ulanguzi wao. Je, ni watu gani wasio na utu kiasi cha kuuza watu wao kwa watu wengine wa mbali?
4 COMMENTS
Donec suscipit porta lorem eget condimentum. Morbi vitae mauris in leo venenatis varius. Aliquam nunc enim, egestas ac dui in, aliquam vulputate erat.