Leo si Kesho

Leo si Kesho

  • Writen byGitau Nduta
  • Year2022

Idili alikuwa kondeni adhuhuri hiyo akiwa na baba yake Bwana Rajua. Jua la utosi lilichoma tosi zao bila chembe ya shufaka. Kijasho chembamba kiliwatiririka tiriri kwa ghadhabu na hamaki. Kijasho ambacho kililovya chepechepe mademu waliyoyavaa. Jasho ambalo walilifuta kwa ncha ya vidole vyao.

Kwa yakini, ni kana kwamba jua lilikuwa limeongezwa makaa kama wenyeji walivyokuwa na mazoea ya kudhukuru. Aghalabu, wenyeji walisikika wakidai kuwa majaliwa yalikuwa yameshika hatamu kuwaadhibu. Adhabu ambayo iliwaacha wakiwa wanyonge wasijue la kufanya. Hata hivyo, enzi za mababu, mandhari ya pale yalikuwa ya kuvutia. Miti ilikuwa imepandwa katika maeneo mengi. Hivyo basi, janibu hii haikuwahi kuhisi ukali wa jua. Aidha, mvua haikuchelewa kupusa hasa msimu wa kifuku. Hivyo basi, chakula kikawa maridhawa nao wakazi wakazidi kuimarika kiafya ila katika ulimwengu wa sasa, kitumbua tayari kilikuwa kimeingia mchanga.

Licha ya joto jingi, wawili hao walilima mgunda huo kwa idili za mwanasheria atafutaye neno la ushindi katika kesi. Huenda walikumbatia falsafa kuwa ajizi ajizi nyumba ya njaa. Si mtu hula jashole? Hii ilikuwa siku ya nne mtawalia katika kibarua hicho. Mwajiri wao Bwana Kandamiza alikuwa nduli asiye na utu licha ya kupambaukiwa na kauli kuwa mtu ni utu. Huyu alikuwa adinasi tofauti na walimwengu wengine. Mara nyingi aliwabeza na kuwatweza kama masuo kisa na maana ukata uliowakata na kuwaacha na makovu tumbi. Sikwambii ni mara ngapi Bwana Kandamiza alisusia kuwapa haki yao; vijisenti kichele kwa kudai kuwa hawakulima kama ilivyotakikana. Vihela ambavyo havikuweza katu kukidhi wala kutosheleza mahitaji yao ya kimsingi. Aghalabu, Bwana huyo alishikilia kikiki kuwa waliacha magugu na visiki mgundani. Kwa kawaida, jambo hilo liliatua mioyo baba na mwana wake. Hata hivyo, hawakuwa na jingine ila kumeza mrututu na kuitikia kurudia kulima shingo mkingamo kwani ni Bwana Kandamiza tu aliyekuwa na nafasi pale kariani Sokomoko; wanakijiji wengi waliupata mkate wao wa kila siku pale kwake. Yeye ndiye aliyekuwa na sauti na satua kitongojini. Alikuwa sawa na kisiwa cha utajiri katika bahari iliyoshamiri mawimbi ya uhawinde....


Book Title Leo si Kesho
Author Gitau Nduta
Date Published January 1st Sat 2022
Chapters 10
Genre Contemporary Fiction
Age Gate 5
Tags African Literature African Ink Nairobi Best seller Fiction

4 COMMENTS

  1. Michel Poe says:

    Donec suscipit porta lorem eget condimentum. Morbi vitae mauris in leo venenatis varius. Aliquam nunc enim, egestas ac dui in, aliquam vulputate erat.

    1. Celesto Anderson says:

      Donec suscipit porta lorem eget condimentum. Morbi vitae mauris in leo venenatis varius. Aliquam nunc enim, egestas ac dui in, aliquam vulputate erat.

  2. Donec suscipit porta lorem eget condimentum. Morbi vitae mauris in leo venenatis varius. Aliquam nunc enim, egestas ac dui in, aliquam vulputate erat.

  3. Donec suscipit porta lorem eget condimentum. Morbi vitae mauris in leo venenatis varius. Aliquam nunc enim, egestas ac dui in, aliquam vulputate erat.

LEAVE A REPLY

Related Books

The Last Hand of Ramogi
  • Contemporary Fiction
Ksh 649
View Details
Pandashuka
  • Contemporary Fiction
Ksh 549
View Details
Afueni
  • Contemporary Fiction
Ksh 349
View Details

Subscribe our newsletter for newest books updates