MGUU NIPONYE

MGUU NIPONYE

  • Writen byDENNIS SHONKO
  • Year2023

Nikwambie mapema, nawe usifikiri nakudanganya ninaposema nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wenye akili za sumaku, wala usiseme ninatia chumvi! Sipingi, kuna wakati nilinyakua nafasi ya pili kwenye tathmini za mitihani, ila si chini ya hapo. Nilijaribu sana kuwa kama wengine wenye nafasi za hali shuleni lakini changamoto zilikuwa nyingi ajabu. Ungeuona mkururo wa watoto ukiingia skulini kila asubuhi ungefikiri sote tulitoka katika familia moja.


Jina langu lilijulikana karibu na wanafunzi wote. Walimu nao hawakuachwa nyuma. Niligundua baadaye kwamba jina Mwamba Muthoni ndilo lililowachekesha. Bila shaka wapo waliojitia hamnazo. Jina Muthoni lilikuwa la mama yangu. Kule kutomjua baba mzazi ndiko kuliniachia jina hilo. Nilikejeliwa hadi nikazoea. Sikuona aibu tena kuitwa Wa Muthoni badala ya Mwamba, bora nikue. Mavazi yangu yakawa kichekesho walipoona nimezoea. Sare zangu zilijaa viraka. Kaptura iliraruka makalioni, ungefikiri ni taa. Sweta iliraruka kwenye kisugudi, hivyo kuonekana kama kinachochungulia. Ukosi wa shati ulikuwa umefika mwisho wa uzee. Viatu? Aa-aa, vilicheka na kunikana! Nilipomwambia mama kuhusu masaibu yangu, alitumia kipaji cha ushonaji vilivyo! Kosa lilikuwa nyuzi za rangi tofauti alizotumia. Vitambaa alivyotumia viliacha mavazi yakiwa kama bendera.


Book Title MGUU NIPONYE
Author DENNIS SHONKO
Date Published February 1st Wed 2023
Chapters 10
Genre Contemporary Fiction
Age Gate 10
Tags African Ink African Literature Fiction Nairobi Best seller

4 COMMENTS

  1. Michel Poe says:

    Donec suscipit porta lorem eget condimentum. Morbi vitae mauris in leo venenatis varius. Aliquam nunc enim, egestas ac dui in, aliquam vulputate erat.

    1. Celesto Anderson says:

      Donec suscipit porta lorem eget condimentum. Morbi vitae mauris in leo venenatis varius. Aliquam nunc enim, egestas ac dui in, aliquam vulputate erat.

  2. Donec suscipit porta lorem eget condimentum. Morbi vitae mauris in leo venenatis varius. Aliquam nunc enim, egestas ac dui in, aliquam vulputate erat.

  3. Donec suscipit porta lorem eget condimentum. Morbi vitae mauris in leo venenatis varius. Aliquam nunc enim, egestas ac dui in, aliquam vulputate erat.

LEAVE A REPLY

Related Books

The Last Hand of Ramogi
  • Contemporary Fiction
Ksh 649
View Details
Pandashuka
  • Contemporary Fiction
Ksh 549
View Details
Afueni
  • Contemporary Fiction
Ksh 349
View Details

Subscribe our newsletter for newest books updates