BAADA YA DHIKI
-
Writen byALEX BARASA
- Year2022
Nimeketi katika chumba cha mhadhara nikiwa nimezama katika bahari ya luja. Kujishika tama kwangu kwa mkono wangu wa kushoto kunaashiria mengi kwa wanaoyatumia macho yao vizuri humu chumbani. Nimezongwa na mseto wa mawazo. Ninawaza zaidi juu ya ulitima unaonitawala mithili ya simba kwenye himaya yake. Mawazo haya yanaufukuzilia mbali kabisa umakini wangu humu darasani.Wakati huo mhadhara wa kozi ya Saikolojia ulikuwa ukiendelea.
Nilikuwa na njaa na nilishinda nikienda miayo kila wakati. Wanafunzi wenzangu waliajabia na kuchukizwa na kitendo hicho cha mimi kwenda miayo madhali ilikuwa bado asubuhi. Asubuhi niliyoinunia na kuichukia kadri ya uwezo wa moyo wangu. Walikiona kuwa kioja cha shani walichosuudika kukiona mara moja tu tangu kuzaliwa kwao. Chausiku na Rehema walikuwa baadhi yao. Nilikuwa nimelala njaa kutokana na kutokuwa na mafuta ya stovu, mafuta ambayo yangeniwezesha kupika. Aidha, asubuhi hiyo sikuwa nimepata kiamshakinywa. Wengi walishinda wakiniangalia kwa nyuso zilizodhihiri kukirihishwa nami. Wengine walisonya kwa bezo.
"Akh! Huyu naye ana nini? Au anataka kutumeza? Anashinda akipanua mdomo na kutuonyesha meno yake meusi tititi kama makaa, meno ambayo hata sijui ni lini mwisho alipiga mswaki!" Chausiku alinong'ona.
Rehema alidakia huku akichekacheka kwa kejeli, "Chausiku, kumbe mimi nina heri! Mbali na kuyaona meno yake machafu, nimeneemeka kuona pia koromeo yake iliyokauka na kukaukiana na kuwa yabisi kama ardhi ya jangwani!"
4 COMMENTS
Donec suscipit porta lorem eget condimentum. Morbi vitae mauris in leo venenatis varius. Aliquam nunc enim, egestas ac dui in, aliquam vulputate erat.